Historia Yetu

Solaris Tanzania Ilianzishwa mwaka 2014 ili kusaidia changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme katika maeneo ya vijijini.

kampuni inahudumia wateja ambao kwa namna moja au nyingine hawana uwezo wa kupata nishati hii kwa shilingi 5000 tu kwa wiki.

Huduma zinatolewa kulingana na uhitaji wa mteja- kuanzia kwenye uhitaji wa taa kwa ajili ya mwanga hadi uhitaji wa mitambo mikubwa ambayo inaweza kuendesha vifaa ambavyo vinaweza vikatumiwa kwenye biashara au kuunganisha jamii kwa pamoja.

Zaidi ya watu wawili miongoni mwa watu watatu katika nchi za Afrika zilizopo chini ya jangwa la sahara zinapata changamoto ya nishati ya umeme.

 Solaris Tanzania inashirikiana na kampuni ya Solaris Offgrid iliyopo nchini Hispania ambayo inatengeneza na kusanifu vifaa pamoja na programu mbalimbali zinazotumika katika kufanya shughuli zote. Solaris Tanzania na Solaris Offgrid zimeweza kuunda ufanisi wa kipekee, uliochangiwa na mbinu itumikayo ya kutengeneza vifaa kulingana na matumizi ya jamii husika. 

Mifumo ya sasa ya kuzalisha nishati ya mwanga ni ya gharama, hupoteza muda na mara nyingi huwa na madhara hasi kwa afya na mazingira. 

Vifaa vyetu vinakupatia mwanga, mawasiliano, fursa za biashara pamoja na burudani kwa jamii. Tunahakikisha kuwa vifaa vyetu ni vya gharama nafuu na mteja wetu anauhuru wa kuchagua jinsi atakavyo fanya malipo; kama ni kwa fedha taslimu au kuchukua mkopo na kurejesha fedha kidogo kidogo hadi miaka mitatu.

Mafanikio Yetu 

Hadi sasa tumefanikiwa kufikisha huduma ya nishati ya umeme safi na wenye gharama nafuu kwa zaidi ya kaya 10,000 ndani ya mikoa ya Tanzania iliyopo kanda ya ziwa. Vilevile tumeboresha maisha kwa zaidi ya watu 200 waliokuwa na uhitaji wa njia za kujikimu kimaisha. 

  • Facebook - White Circle
  • Twitter - White Circle
  • YouTube - White Circle
  • Instagram - White Circle

Copyright © 2019 Eternum LTD T/A Solaris Tanzania, All rights reserved